Rais wa Uganda, Yower Museven.
Raia wa Uganda kutoka dini mbali mbali hii leo wamekusanyika katika uwanja wa Kololo mjini Kampala kwa maombi maalum na kutoa shukrani kwa Rais Yoweri Museveni kwa kutia saini muswada wa sheria inayozuia mapenzi ya jinsia moja.
Rais Museveni aliidhinisha sheria hiyo inayotoa adhabu kali kwa Mashoga nchini Uganda mwezi Februari, kwa hatua hiyo viongozi wa dini mbalimbali wakristo na waislamu wamehimiza waumini wao kujitokeza kwa wingi katika ibada hiyo maalum.
Hii ni mara ya kwanza viongozi wa dini mbali mbali nchini Uganda kujitokeza kwa pamoja na kuandaa Ibada maalum ya kumshukuru Rais Museveni na kuliombea taifa kuepuka vitendo vya ushoga.
Rais Museveni aliidhinisha sheria hiyo ambayo raia wengi wa Uganda wameipigia debe sana.
Ibada hiyo maalum inafanyika uwanja wa uhuru wa Kololo mjini Kampala, baada ya karibu mwezi mmoja na nusu tangu rais Yoweri Museveni kuiidhinisha
Tangu Rais Museveni kuidhinisha sheria hiyo kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi yakimtaka kubadili msimamo wake, huku baadhi ya mataifa yakipunguza msaada kwa Uganda lakini raia wengi wa Uganda walimsifu Rais Museveni kwa hatua yake.
Chanzo, bbcswahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni