A
Kundi la al-Shabab
nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya jeshi la Kenya chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom) nchini
Somalia.
Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye
shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na
mpaka wa nchi hiyo na Kenya."Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya mapigano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameliambia shirika la habari la Reuters.
Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Naye Kanali Paul Njuguna ameiambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."
Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.
Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake mjini Mogadishu.
Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi yajeshi la Kenya ya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.
Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni