Mtu mmoja katika
jimbo la Masachussets nchini Marekani ameshtakiwa kwa tuhuma za
kutekeleza uhalifu wa chuki baada ya kumpiga teke mfanyakazi Muislamu
katika uwanja wa ndege wa JFK pamoja na kumkaripia.
Robin Rhodes
mwenye umri wa miaka 57 anatuhumiwa kwa kusema Trump....atawafukuza
nyinyi nyote na baadaye akamzuia mwanamke huyo kutoondoka katika ofisi
yake.Kushambulia na kuwazuilia watu ni miongoni mwa mashtaka ya uhalifu wa chuki ambao mtu huyo kwa sasa anakabiliwa nayo, kulingana na hakimu wa Queens District.
Anakabiliwa na kifungo cha miaka 4 jela iwapo atapatikana na hatia.
Mfanyakazi huyo wa kampuni ya ndege ya Delta Airlines ambaye alikuwa amevaa hijab alikuwa ameketi katika ofisi yake siku ya Jumatano wakati Rhodes alipodaiwa kwenda katika mlango wake na kuanza kumkaripia, kugonga mlango, kumzuia kuondoka na kumpiga teke.
Wakati mtu mwengine alipoingilia kati na kumsaidia mwanamke huyo kutoka ofisini mwake, mtu huyo alidaiwa kumfuata na kupiga magoti mbele yake akiigiza maombi ya kiislamu.
''Islam na Isis, sasa Trump amewasili. Atawafurusha nyote. Unaweza kuuliza Ujerumani, Ubelgiji na Ufaransa kuhusu watu hao.utaona kilichojiri''.
Pia ameshtakiwa kwa kupiga kelele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni