Maelfu ya watu wamehudhuria sherehe za kukabidhiwa mamlaka kwa
Rais mpya Peter Mutharika.
Bwana Mutharika, alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi jana. Uchaguzi huo
ulikumbwa na madai ya wizi wa kura.
Rais anayeondoka mamlakani Joyce Banda, alishika nafasi ya tatu katika idadi
ya kura za urais.
Viongozi kadhaa kutoka Afrika walihudhuria sherehe hizo katika uwanja wa
Kamuzu, mjini Blantyre.
Mtangulizi wake Mutharika, Joyce Banda alisusia sherehe hizo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza ambaye yuko mjini Blantyre, anasema kuwa
serikali ilitoa mwaliko kwa wakuu wa nchi kadhaa za Afrika wakiwemo majirani
zake wote ili kushuhudia hafla hiyo muhimu.
Jumamosi asubuhi Jaji mkuu Anastazia Msosa alimwapisha Mutharika kuwa Rais wa
tano wa Malawi ikiwa ni saa 12 tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu
uliokuwa umejaa malalamiko ya wizi wa kura na pingamizi mahakamani.
Akizungumza nyumbani kwake mara baada ya kula kiapo Rais Mutharika amewaahidi
wamalawi uhudumu bora na kumaliza kiu yao ya maendeleo, huku akiwataka wapinzani
wake katika mbio za urais akiwemo Dr Joyce Banda waungane naye kuijenga
Malawi.
Hata hivyo Dr Banda pamoja na wagombea urais wengine kumi na moja walioshindwa,
wamempongeza Rais mpya na kuwataka wafuasi wao kukubali matokeo na kujipanga
upya kwa uchaguzi ujao wa mwaka 2019 (BBC)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni