Mfalme wa Uhispania Juan Carlos anaachia mamlaka, waziri mkuu
Mariano Rajoy ametangaza.
Juan Carlos, mwenye umri wa miaka 76, amekuwa mfalme tangu mwaka 1975 , baada
kumrithi aliyekuwa dikteta Francisco Franco.
Mwanawe mfalme, Felipe, 45, ndiye atakayemrithi.
Katika kipindi cha utawala wake, Juan Carlos alionekana kama mfalme mwenye
umaarufu sana duniani, lakini hivi karibuni, wananchi wengi wa Uhispania
walipoteza imani nae.
Sifa yake imetiwa dosari kufuatia uchunguzi wa muda mrefu wa madai ya ufisadi
dhidi ya mtoto wake wa kike na mumewe.
Uungwaji mkono kwa mfalme huyo ulizorota zaidi ilipogundulika kuwa alikuwa
katika safari ya kuwinda Ndovu nchini Botswana mwezi Aprili 2012 wakati nchi
hiyo ilipokuwa inazongwa na msukosuko wa kifedha.
Mfalme Juan amendoka mamlakani kwa sababu zake binafsi.
Hali yake ya kiafya, sio nzuri sana na amefanyiwa upasuaji mara kadhaa katika
miaka ya hivi karibuni.
Waziri Mkuu hata hivyo alisema kuwa mfalme Juan Carlos amekuwa mtetezi wa
haki za watu wa nchi hiyo(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni