Jumatano, 22 Aprili 2015

MISHIKAKI YA CHURA HII HAPA

Philip Paul mfanyabiashara wa mishikaki ya chura katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria
Kwa wapenzi wa kula nyama choma na hususan mishikaki katika vituo vya mabasi, mnatakiwa kuwa makini na nyama choma hiyo kwani waweza kula mishikaki ya paka, mbwa, nyoka na sasa mishikaki ya nyama ya chura.
 
Mishikaki ya nyama ya chura
Philip Paul ni muuzaji wa nyama choma za chura - na yeye pamoja na mke wake na mtoto wao wa kike wanapenda kula mishikaki ya chura. Familia hiyo inatoka jimbo la katikati ya Nigeria la Benue lakini wanaishi kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambako watu hawapendelei nyama hii ya chura.
Philip mwenye umri wa miaka 25 anasema ni rahisi kuwakamata vyura kwa mikono mitupu. Usiku anawatega kwa kuwawekea popo na vyura wanaporuka huwaendea na kuwakamata.
Baadaye anawatunga katika mti. Tangu mwaka 2008 amekuwa akifanya biashara kwa kuwakamata vyura katika jimbo la Adamawa na kuwasafirisha kwenda jimbo la Benue, ambako mishikaki ya chura inapendwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni