Timu
nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani
Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na
Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.
Wakicheza katika uwanja wao wa
nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika
ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez
almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico
Madrid.Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni