Jumatano, 2 Julai 2014

MTATIRO AFUNGUKA


ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro.

Jackson Odoyo, Dar es Salaam
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro amesema kwamba yeye hawezi kuwa malaya wa siasa kiasi cha kubabaishwa na propaganda zinazo enezwa kwamba, ameamua kutogombea nafasi yoyote katika Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho kwa sababu ya tamaa ya uongozi.


Akizungumza na Habarimpya.com Mtatiro amesema kwamba hakuwahi kufikiri kwamba anauwezo wa kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wala nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho kwa sababu bado hana uwezo na ni mchanga katika siasa, kwani hata umri wake bado ni mdogo sana hivyo hawezi kufikiria nafasi hizo kwa sasa.

"Kuna propaganda zimeanza kuelezwa juu yangu mengi yanasemwa lakini mimi ndiyo najua sababu na sababu yenyewe ni kwamba nina majukumu ya kijamii na kifamilia ambayo yananikabili kwa sasa, niko masomoni ninatakiwa kuwa darasani muda wote wakati mwingine napaswa kuwa masomoni kuanzia asubuhi mapaka jioni, hivyo nisingeweza kufanya mambo mawili mazito kwa wakati mmoja" anasema Mtatiro na kuongeza:

"Mfano nilikuwa na nafasi ya kushinda katika nafasi yangu ya Naibu Katibu Mkuu, lakini ni nafasi ambayo inamtaka mtu kwenye muda wa kutosha kuitumikia Chama, hivi sasa CUF inajiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa, na Uchaguzi Mkuu, na mimi nitatakiwa kuwa masomoni mpaka mwezi Julai mwakani, hivyo nisingeweza kukitumikia Chama ipasavyo.

Mtatiro amefafanua kwamba kama kuna watu wameanza kuvumisha kwamba anaweza kuhamia vyama kama ACT na vingine wanajidanganya kamwe hawezi kuharibu kiwango chako cha uongozi, amejifunza mambo mengi kutoka kwa Profesa Lipumba na Maalim Sefu na kamwe hakuwahi kugombana na viongozi hao hata siku moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni