Jumamosi, 10 Mei 2014

JK AANZA ZIARA DRC

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maua muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ndjili jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) Augustin Matata Ponyo Mapon akimkaribisha na kuzungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika mji mkuu wan chi hiyo Kinshasa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Rais Kikwete baada ya atakutana na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila na kufanya naye mazungumzo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) Mh.Anthony Ngereza Chehe aliyelazwa katika hospitali ya Ngaliema Health Centre jijnii Kinshasa baada ya kuugua malaria.Rais Kikwete yupo jijini Kinshasa DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni