Kigugumizi ni hali ambayo mtu anashindwa kuongea moja kwa moja, kukwama kutamka neno, kurudiarudia neno au kuacha kuongea kabisa. Hali hii inawakumba watu kiasi cha milioni 70 dunia nzima. Hakuna sababu moja inayosababisha tatizo hili. Baadhi ya machapisho yanasema kuwa tatizo linatokana na baadhi ya neva (nerves) kushindwa kuwasilisha au kupeleka taarifa moja kwa moja, kurithi ambapo wanasema mtoto mwenye wazazi wenye kigugumizi ana uwezekano mkubwa wa kuwa na kigugumizi nk
.
Ni tatizo ambalo linahusu kushindwa kuongea moja kwa moja lakini pia kuna wanaoshindwa kuongea kabisa. Mara nyingi watu wa aina hii wanakuwa na hasira sana. Wakati mwingine wakikutana na mtu mwenye kigugumizi wanakasirika sana wakidhani wanawatania.
Mwanzoni unaweza kumgundua mtu mwenye kigugumizi kwa kurudia herufi kwa mfano u-u-u-naju- ju-jua, hahahaa- bari yayayaa-ko nk.
Matibabu:
Kwa hapa nchini sina uhakika kama tuna madaktari bingwa wa taaluma ya kuzungumza (speech) lakini kwa nchi za Ulaya kuna watu waliosome na kubobea na kuitwa certified speech-language pathologist (SLP).Ila kama una tatizo la kigugumizi au mwanao unshauriwa kufanya yafuatayo:
- kujaribu kujizoeza kutamka neno moja moja
- baada ya hapo ujaribu sentensi fupifupi
- ujaribu kujizoeza kuzungumza taratibu
- ujaribu pia kujizoeza kupumua taratibu
- kujaribu kupunguza hasira
sawa nitajarbu
JibuFutaPia jaribu kuzungumza mbele ya watu weng
JibuFutaSawa nitajaribu
JibuFuta