Kundi la wanamgambo
la al-Shabab la nchini Somalia, limethibitisha kuwa limewaua wanaume
wanne waliolaumiwa kwa kuipelelezea Marekani, Kenya na serikali ya
Somalia inayoungwa mkono na nchi za magharibi.
Wanaume hao walikatwa vichwa hadharani kwenye mji ulio wilaya ya
Jamame eneo la Jubba karibu kilomita 70, kaskazini mwa mji wa Kismayo
baada ya kupatwa na hatia na mahakama ya Sharia.Wanaume hao walikiri kuwa walikuwa wapelelezi, kwa mujibu wa shirika la Reuters, lililomnukuu gavana wa al-Shabab Abu Abdalla, eneo la Jubba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni