Mahakama ya juu nchini Libya imesema kuwa kuchaguliwa kwa Ahmed
Maiteg kama waziri mkuu mwezi uliopita ulikiuka katiba ya taifa hilo.
Maiteeg aliyeapishwa kuwa Waziri mkuu mwezi uliopita na bunge la taifa ,baada
ya kura iliyokumbwa na utata.Hata hivyo taifa hilo limegawanyika kati ya waislamu wa kadri na wale wenye misingi kali ya dini.
Milengo hiyo ya waislamu ndiyo yanayodhibiti maeneo tofauti ya Taifa hilo.
Uchaguzi unatarajiwa kufanyika terehe 25 June,kuchagua bunge la taifa litakalorithi nafasi inayoshikiliwa kwa sasa na kongamano la kitaifa al maarufu '' General National Congress''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni