Mwanaume mmoja na Mwanamke mmoja walifariki eneo la tukio na wawili walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wakati majeruhi wanane walikimbizwa Rufaa kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na juhudi za kumtafuta Dereva wa lori zinaendelea.
Aidha amewataka wamiliki wa magari na madereva kuyafanyia matengenezo na ukaguzi wa mara kwa mara magari yao ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Mbeya Ifisi, Sikitu Mbilinyi amewataja majeruhi kuwa ni Dereva Fred, Maiko Malema(16), Justin Komba(24), Amir Ramadhan(26), Nausi Bakari(28), Jackson Kambo(19), Anoria Ndezi(13) na Lucy Edson(17).
Mbilinyi amewataja wengine kuwa ni Groly Paul(27), Moyo Safi (1), Rahma Peter(3), Mary Kitine(57), Mariam, Karen Naiman, Mecy, Adelina Malipesa(52), Suzana Athas(35), Adelina Essau(28), Flora Essau(64) na Emmy Charles(21).
Wengine waliolazwa ni pamoja na Diana Jumbe(19), Esther Seleman(21),P aul Mayeta(45)ambaye ni Dereva msaidizi, Bahati Julius(33) na Joseph Komba(34).
Kwa mujibu wa Muuguzi Mkuu hali za majeruhi zinaendelea vizuri na wanafanya kila jitihada za kuokoa maisha yao na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu kwani Hospitali hiyo ina uhitaji mkubwa kutokana na kuwa karibu ya barabara kuu na ajali zinazojitokeza mara kwa mara ingawa hupatiwa damu kutoka Benki ya Damu salama.
Hata hivyo baadhi ya abiria wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wananchi wa Nanyala badala ya kusaidia majeruhi walikuwa wakiwapora mizigo, simu na fedha pia waliokuwa na vito vya thamani kama hereni.
Jackson Kambo ambaye ni mmoja wa wahudumu wa basi hilo amesema kuwa kama wananchi hao wangetoa msaada mapema kondakta wake asingefariki lakini badala ya kusaidia walikuwa wanang'ang'ania mkoba wa fedha hadi walipofanikiwa kuchukua fedha ndipo walianza kutoa msaada marehemu akiwa amelaliwa mkono na basi.
Kambo amesema kama si juhudi binafsi Dereva wa basi angepoteza maisha kutokana na kubanwa na mkanda hivyo kulazimika kuukata na kuanza kusaidia kuokoa abiria wengine.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni