Machafuko
yaliyotokea nchini Misri.Mahakama nchini Misri imemuhukumu adhabu ya
kifo aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Mohammed Morsi kwa kosa la
kuchochea machafuko wakati wa maandamano Desemba mwaka 2012 yaliyolenga
kupinga uongozi wake.
Mohammed
Morsi alikutwa na hatia hiyo baada ya kukamatwa waandamanaji waliokuwa
wakipinga serikali yake, hivyo jeshi kumtimua madarakani Julai 2013.
Mohamed
Morsi alishirikishwa katika kesi hiyo pamoja na viongozi na wafuasi
wengine 12 wa Kundi la Kiislam Muslim Brothehood, ambao mwanzoni (mwezi
uliopita) walihukumiwa pia kifungo cha miaka 20 jela.
Morsi ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza (rais) aliyechaguliwa kwa njia kidemokrasia nchini Misri licha ya kuhukumiwa kifo.
Waendesha
mashtaka wanamtuhumu Mohamed Morsi na viongozi wengine wa Muslim
Brotherhood kuchochoea machafuko yaliyosababisha mamia ya waandamanaji
nchini Misri kufariki dunia Desemba mwaka 2012.
Hisia
tofauti zimetolea nchini Misri baada ya uamzi huo wa Mahakama kutangazwa
na jaji mmoja wa mahakama ya nchi hiyo, Shaaban el-Shami.
Raia
wanaomuunga mkono Mohamedi Morsi wamepokea kwa shingo upande uamzi huo.
Wengi walidhani kwamba rais huyo wa zamani wa Misri angepunguziwa adhabu
yake ya mwanzo ya kifungo cha miaka 20 jela.
Kwa
upande wao raia wasiomuunga mkono wamenukuliwa wakisema kuwa hukumu
aliyopewa inafaa ikilinganishwa vitendo alivyovifanya wakati akiwa
madarakani.
Kwa
upande wao, wafuasi wa Muslim Brotherhood ambao wamezungumza na vyombo
vya habari vya kigeni na vile vinavyopeperusha kwenye mitandao
mbalimbali, wamebaini kwamba kesi hiyo ni ya kisiasa, ambayo imekua
ikiandaliwa na kundi la wanajeshi waliohusika katika kuupindua utawala
wa Morsi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni