Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewasili katika
mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo anakutana na rais Hassan Sheikh
Mohamud, viongozi wa eneo la Afrika mashariki pamoja na mashirika ya
kijamii.
Ni waziri wa kwanza wa kigeni kutoka Marekani kuutembelea mji huo. Kerry hataondoka katika uwanja wa ndege wa mji huo unaolindwa sana.Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani inataka kutoa ujumbe kwa kundi la Alshabaab kwamba halipatii kisogo taifa la Somalia.
Marekani imetoa mamia ya madola nchini Somalia katika siku za hivi karibuni.
Ndege zisizokuwa na rubani za Marekani zimewaua viongozi kadhaa wa kundi la Alshabaab.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni