Jumanne, 5 Mei 2015

MAHAKAMA YA BURUNDI YAMRUHUSU NKURUNZINZA KUGOMBEA URAIS

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Kulingana na vituo vya redio nchini humo, Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .

Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse, alirpotiwa kutoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.

Hata hivyo serikali ya Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.

Uamuzi huu huenda ukachochea maandamano zaidi ya wananchi wanaopinga rais huyo kuongezewa muhula wa tatu ambapo maandamano hayo hadi sasa yameshasababisha vifo vya wananchi 9 na wengine kadhaa kujeruhiwa. Tayari wakimbizi wameingia nchi jirani za Tanzania, Rwanda na DRC kukimbia machafuko hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni