Mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA mh FREMAN MBOWE
amewasili leo katika stendi ya mabasi Ubungo kuzungumza na madereva ambao
walikuwa wakiendea na mgomo wa kuitaka serikali iwasikilize shida zao. Mh
Mbowe ambaye aliwasili hapa majira ya saa nne kasoroo asubuhi alijikuta
katika wakati mgumu baada ya wananchi kumshangilia kwa nguvu huku
wengine wakifungua barabara ili gari yake ipite huku nyimbo za UKAWA
zikiimbwa, jambo ambalo lilizua taharuki katika eneo hilo.
Mbowe akihutubia madereva
Mh mbowe
alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa madereva hao. Aidha viongozi
kadhaa wa serikali waliokuwa katika eneo hilo walionekana kuzomewa na
kutokuaminika na madereva hao.
Kuhusu mgomo huo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh Paul Makonda amewaomba
madereva hao kuendelea na kazi na ndani ya siku saba serikali itakuwa
tayari imeshatoa tamko.
Madereva hao wamekubali kuanza safari kwa sharti la ndani ya siku saba
wawe wamesikilizwa kero zao.MH MBOWE alipotaka kuzungumza na madereva hao microfone zote zilizimwa na kufichwa kusikojulikana jambo ambalo lilifanya ashindwe kusikika kwa madereva hao na kuamua kumtoa nje na kusukuma gari yake hadi maeneo ya Shekilango na kurudi ofisini. Taarifa ni kuwa mgomo huo umekwishwa na magari hapa Ubungo yameanza kuondoka kuelekea mikoani japo kwa kuchelewa sana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni