Jumatano, 27 Septemba 2017

Mwanamke ajioa mwenyewe nchini Italia

Laura Mesi, who married herself, cuts her wedding cake

 Furaha yangu haitegemei uwepo wa mwanamume
Mwanamke mmoja nchini Italia amejioa yeye mwenyewe kwenye sherehe iliyokuwa na vazi kamili la harusi, keki na wageni 70.
"Ninaamini kuwa kila mmoja wetu ni lazima ajipende," alisema Luara Mesi mwenye miaka 40
Wanaounga mkono ndoa kama hizo wanasema kuwa suala kuu ni kujipenda.

Laura anasema kuwa suala la kujioa lilimjia miaka miwili iliyopita, baada ya miaka 12 ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

  Laura Mesi and her bridesmaids
Ndoa ya Bi Mesi
"Niliwaambia marafiki zangu na familia kuwa sijapata mpenzi na kama nikifikia umri wa miaka 40 bila mchumba nitajioa." aliliambia gazeti la La Repubblica.
"Ikiwa siku moja nitapata mwanamume ambaye nitapanga kuishi naye nitafurahi, lakini furaha yangu haimtegemei yeye."
Bi Mesi anasema kuwa yeye ndiye mwanamke wa Kwanza nchini Italia kufanya harusi ya mtu mmoja.
  Carved watermelon at the solo wedding of Laura Mesi
Tunda la kusherehekea ndoa ya Laura Mesi
Kati ya maoni yaliyowekwa kwenye picha za Bi Mesi ni pamoja na , "vibaya sana", "umechanganyikiwa" na "kuna tatizo na ubongo wako."
Hata hivyo Bi Mesi ametupilia mbali maoni hayo akisema hakuna mtu atakayezima tabasamu lake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni