Shirika
la afya duniani WHO, limesifia matokeo ya chanjo mpya ugonjwa wa Ebola, inatoa asilimia 100% ya kinga baada ya majaribio yake nchini
Guinea.
WHO linasema kuwa ulimwengu unakaribia zaidi kupata chanjo mpya dhidi ya ugonjwa huo hatari wa Ebola.Dawa ya chanjo hiyo ilijaribiwa maelfu ya watu, mara tu mtu mmoja aliyekuwa karibu nao alipoambukizwa ugonjwa huo, lakini baada ya kutibiwa kwa siku kumi hakuna hata mmoja wao aliyekuwa ameambukizwa ugonjwa huo.
Licha ya kuwa chanjo hiyo bado haijaidhinishwa rasmi ama kupewa leseni, tayari maandalizi yanafanywa ili isambazwe wa kote Duniani.
Zaidi ya watu elfu kumi na moja wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa ebola, tangu ulipolipuka nchini Guinea mwezi Disemba mwaka 2013
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni