Kwa mujibu wa taarifa ya familia ya Mrema aliyekuwa pia mmilikiwa hoteli za Impala ya Moshi na Arusha, Naura Springs ya Arusha na kampuni kadhaa za utalii, nyumba na magari ya kukodisha, mwili wa bilionea huyo utazikwa Jumatano ijayo nyuma ya hoteli yake ya Ngurdoto iliyopo Usa River, wilayani Arumeru. Taarifa hiyo ilisema kuwa mwili wa Mrema unatarajiwa kuwasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) majira ya saa 7 mchana.
Baada ya kuwasili, mwili huo utapelekwa moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospital ya Rufaa ya Seliani inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Arusha. Taarifa hiyo imesema Jumanne mwili huo utapelekwa nyumbani kwake eneo la Uzunguni kwa ajili ya ibada .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni