Eman Ahmed Abd El Aty
Mwanamke mmoja raia
wa Misri anayeaminiwa kuwa mtu mzito zaidi duniani akiwa na kilo 500,
hivi karibuni atasafirishwa kwenda nchini India kufanyiwa upasuaji wa
kupunguza uzito wake.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka
36, atasafirishwa kwa ndege ya kukodishwa kwenda mjini Mumbai, ambapo
daktari Muffazal Lakdawala, anapanga kumfanyia upasuaji.Ubalozi wa India mjini Cairo ulikuwa umemnyima visa kwa kuwa hakuweza kufika kwenye ubalozi huo yeye binafsi.
Hata hivyo hali ilibadilika baada ya daktari kutoka mji wa Mumbia kuindikia wizara ya mashauri ya Nje ya India kupitia mtandao wa Twitter.
Familia ya bi Abd El Aty inasema kuwa hajaondoka nyumbani kwa miaka 25.
Ikiwa madai kuhusu uzito wake ni ya ukweli basi atakuwa mtu mzito zaidi duniani aliye hai kwa kuwa Pauline Potter aliyekuwa na kilo 272 (ratili 600) mwaka 2010 wa Los Angeles Maekani ndiye anashikia rekosi ya Guinness
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni