Adabu ishike mkondo wake! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose amejikuta akichezea kichapo ‘hevi’ kilichomsababishia kuvunjika pua kwa tuhuma ya ukuwadi wa mke wa mtu, .
“Haiwezekani awe anawakuwadia wake zetu kwa wanaume wengine, leo tulipanga tumtoboe hata jicho moja ili liwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama za Jose,” alisema mmoja wa vijana waliokuwa wakimsulubu jamaa huyo.
Vijana waliokuwa eneo la tukio wakizozana katika songombingo hilo.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwanaume aliyemwekea mtego Jose ambaye aliomba hifadhi ya jina gazetini alisema kwamba, waliamua kumpa mkong’oto kijana huyo baada ya kuchoshwa na vitendo vyake hivyo.
Kwa upande wake Jose alishindwa kusema lolote huku akisikilizia maumivu ya kipigo hadi alipoondolewa eneo la tukio na wasamaria wema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni