Al QAEDA WAUA 14 YEMEN
Wanajeshi wa Yemen
Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al Qaeda kusini
mashariki mwa Yemen wamewateka na kuwaua takriban wanajeshi 14 waliokuwa
wakirudi nyumbani kutoka kazini mashariki mwa taifa hilo.
Wanajeshi hao walidaiwa kuwa katika likizo wakati basi lao liliposhambuliwa
na wanamgambo hao kabla ya kutekwa nyara.
Maafisa katika eneo hilo wanasema kuwa walipata miili yao saa chache baadaye
karibu na mji wa Sieyoun katika mkoa wa Hadramout.
Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wanajeshi wa serikali ya
Yemen yanayotekelezwa na wanamgambo wa kundi la Al Qaeda(Tukuo)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni