Mtandao wa Wikipedia umekataa kufuta picha ambayo Nyani
ilijipiga ikisema kuwa kwa sababu picha hiyo ilipigwa na Nyani ambaye ni mnyama
wala sio binadamu, basi inakuwa mali ya umma.
Hii ni baada ya mpiga picha, mmiliki wa kamera iliyotumika na Nyani huyo
kujipiga picha, kusihi Wikipedia kufuta picha hiyo na kudai kuwa Wikipedia
ilikuwa inaingilia haki zake za umiliki wa picha hiyo.Picha hiyo aliyojipiga Nyani bila shaka ni ya kusisimua na imempelekea David kuwa maarufu ulimwengu mzima.
La kusikitisha ni kuwa hatimaye Slater sasa amejikuta katika mvutano wa kisheria na Wikimedia kuhusiana na ni nani hasa mmiliki wa picha hiyo.
David, ambaye hutegemea upiga picha kama jinsi moja ya kujikimu kimaisha, yuko makini kuhakikisha picha hiyo imeondolewa kwa tovuti ya Wikipedia mara moja, huku Wikipedia ikidai kuwa iwapo kuna mmliki wa picha hiyo basi ni Nyani aliyejipiga picha hiyo.
Mvutano wa kisheria ilirejelewa kuangaziwa kufuatia uamuzi wa Wikipedia kuchapisha maombi yote iliyopata kuhusu kufuta au kuhariri habari au picha au video zozote ilizoweka kwenye tovuti zao.
Mojawapo ya maombi hayo ni David Slater kutaka picha aliyojipiga Nyani kuondolewa kwenye tovuti ya Wikipedia mara moja kwani ikiwa kwenye tovuti hiyo iko wazi kwa umma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni