WATU SITA WAUAWA KWENYE GHASIA SOMALIA
Wapiganaji wa Al-shabaab
Takriban watu sita wameuawa katika ghasia katikati mwa
Somali.
Ijumaa usiku, wanamgambo kutoka kundi la Alshabaab walishambulia kambi moja
ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mji wa Buloburde, yapata kilomita 200
kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.
Vikosi vya Amisom viliuteka mji wa Buloburde kutoka kwa Alshabaab mapema
mwaka huu, lakini wanamgambo hao bado wanadhibiti eneo kubwa la viunga mwa mji
huo.
Wameendelea kutekeleza mashambulizi mjini Mogadishu ili kujaribu kuiondoa
serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa.(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni