Idadi ya watu waliofariki kutokana na Ebola Afrika Magharibi
inasemekana kufika 900
Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa
Ebola Magharibi mwa afrika kama janga la kimataifa linalohitaji kushughulikiwa
kwa dharura.
WHO imesema kuwa mataifa yalio na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hayana
uwezo wa kudhibiti kiwango cha virusi hivyo na hivyo basi yanahitaji usaidizi wa
kimataifa.
Tangazo hilo linajiri baada ya mazungumzo ya dharura mjini Geneva kuhusu
uwezekano wa kutuma wataalam wa ugonjwa wa maambukizi ili kuudhibiti ugonjwa huo
ambao ni hatari zaidi.
Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu mia tisa magharibi mwa afrika .
Mataifa yalioathiriwa vibaya ni Guinea,Liberia na Sierra Leone,lakini pia
visa vimeripotiwa nchini Nigeria
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni