Ndege moja iliyokuwa na abiria 40 imeanguka mjini Tehran nchini Iran.
Luninga ya taifa la Iran imesema kuwa abiria wote wamefariki .
Ndege hiyo ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makaazi ya watu baada
ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Maghribi mwa mji wa Tehran.
Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kupitia
teknologia ya Ukraine.
Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ni nini kilichosababisha ajali hiyo.
Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na
ndege zake zilizozeeka mbali na matengenezo mabaya inazozifanyia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni