VYETI BANDIA VYA UKIMWI VINAUZWA NCHINI UGANDA
Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua
matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi hivyo
nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizonaswa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa
hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria wanasema
wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata
wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alitembelea kliniki 15
bila ya kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya
kuthibitisha kuwa hana virusi vinavyosababisha UKIMWI na VVU.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila
cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo
mengi ya mji mkuu wa Uganda, Kampala zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza
cheti pia kwa urahisi sana.
BBC ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda, ushahidi huo, alikubali
kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila
juhudi kuwakamata na kuwashitaki wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa
kupambana na ukimwi nchini Uganda. Naye Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi
kupambana na kashfa hiyo (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni