MOTO MKUBWA WATEKETEZA SEHEMU LA SOKO MOMBASA
Mombasa, Kenya:
Soko la Kongowea mjini Mombasa limeungua baada ya moto mkubwa kuunguza sehemu ya rejareja ya soko hilo usiku wa kuamkia leo.
Moto huo ambao ulianza saa 6 usiku ulizimwa na kikosi cha zimamoto ambacho kilifika eneo hilo muda mfupi baada ya moto kuwaka. Moto huo ambao umeteketeza mali za mamilioni ya shilingi za Kenya ulizimwa saa 11 alfajiri.
Wafanyabiashara wa soko hilo walionekana asubuhi hii wakihesabu hasara iliyopatikana.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na polisi wananedelea na uchunguzi (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni