Jumapili, 7 Juni 2015

BARCA BINGWA WA UEFA KWA MARA YA 5. YAIFUMUA JUVE MABA0 3-1

Barcelona wakiwa na kombe
Barcelona walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.

 
Barcelona
Hata hivyo Alvaro Morata alisawazisha. Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya gusa ni guse kati yake na Messy.
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.
Barcelona
Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya msimu huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni