Jumapili, 7 Juni 2015

MWANABLOGU ALIYETUSI UISLAM JELA NA VIBOKO ALFU

 
Maandamano ya wanaopinga adhabu kali nchini Saudia
 
Mahakamu kuu nchini Saudia imeamua kuwa hukumu ya kifungo cha miaka 10 na viboko 1000 dhidi ya mwanablogu Raif Badawi aliyepatikana na hatia ya kutukana Uislamu itabaki vile ilivyo.

Utawala nchini Saudi Arabia uliamuru kusikilizwa tena kwa hukumu hiyo kufuatia shutuma za kimataifa baada ya bwana Badawi kuchapwa viboko hamsini mapema mwaka huu.
Mkewe na makundi ya haki za kibinadamu yameonya kuwa huenda akafa ikiwa hukumu hiyo yote itatekelezwa.

Bwana Badawi alikamatwa kufuatia blogi aliyoanzisha ambayo ilikashifu baadhi ya tamaduni nchini Saudi Arabia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni