Mtu mwenye bunduki
amewaua watu saba kwenye nyumba moja mjini Dallas, Texas nchini
Marekani, kabla ya kuuawa kwa kipigwa risasi na polisi.
Watu wawili ambao nao walipigwa risasi wako hospitalini.Msemaji wa polisi David Tilley alisema kuwa mshambuliaji aliuawa na polisi kwa kwanza ambaye aliyefika wakati wa ufyatulianaji wa risasi. Polisi huyo hakujeruhiwa.
Kile kilichochangia shambulizi hilo bado hakijulikani au ikiwa mshambuliaji aliwafahamu waathiriwa bado ni kitendawili.
"Tunajaribu kuangalia suala hili kwa kina," Bwa Tilley alisema.
Gazeti moja huko Dallas liliripoti kuwa wale waliouawa walikuwa wakitazama timu ya Dallas Cowboys, ambayo ni timu ya kandanda ya Marekani wakati waliposhambuliwa.
Polisi hawajatoa jina la mshambuliaji au muathiriwa yeyote lakini wote wametajwa kuwa watu wazima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni