Bilionea Sir Richard akitathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Irma
Sir Richard Branson
amesema mengi ya majengo na mimea na miti katika kisiwa chake cha
Necker katika eneo la Caribbean vimeharibiwa kabisa na Kimbunga Irma.
Necker ni moja ya visiwa 50 ambavyo hujumuisha Visiwa vya British Virgin vya Uingereza (BVI).Sir Richard amesema alitembelea kisiwa kinachokaribia zaidi kisiwa chake cha Necker na kujionea "moja kwa moja ukali na ukatili wa kimbunga hicho".
Kimbunga hicho kiliua watu watano katika eneo hilo la Uingereza.
Waziri mkuu wa BVI ameomba usaidizi wa muda mrefu kutoka kwa Uingereza.
Sir Richard na wenzake wako salama.

Sir Richard amesema: "Tulihisi nguvu kali zaidi za kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kupiga kutoka Bahari ya Atlantiki. Lakini tulikuwa na bahati sana kwamba tulikuwa na handaki imara ambalo tulikuwa tumelijenga katika Jumba Kuu la Necker na tulikuwa na kwamba watu wote waliokuwa kisiwani wakati wa kimbunga wako salama."

Mawasiliano bado yamekatizwa katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Sir Richard kwa sasa yuko katika kisiwa cha Puerto Rico, kilomita kadha magharibi mwa visiwa hivyo vyake.

Sir Richard amesema atazungumza na serikali mbalimbali na mashirika ya misaada, pamoja na vyombo vya habari.
Amesema baadaye atarejea kupigania zaidi kufanywa kikao cha kuchangsha misaada kwa Visiwa vya Virgin vya Uingereza ili kusaidia juhudi za ukarabati.
Visiwa vya Virgin vya Uingereza ni eneo linalojitawala la Uingereza ambalo humtambua Malkia Elizabeth wa Uingereza kama kiongozi wa taifa.
Waziri mkuu wa visiwa hivyo Orlando Smith amesema watahitaji misaada kwa kipindi kirefu kutoka Uingereza.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni