Katika Uchaguzi huo unahusisha nafasi za udiwani, ubunge na urais lakini kuna jambo wagombea wanapaswa kujifunza kutoka kwa rais wa sasa wa nchi ya Uruguay, José Alberto "Pepe" Mujica Cordano ambaye anaishi maisha ya kawaida yasiyo na utofauti na yale ya mwananchi wa kijijini.
Katika haya makala iliyoandikwa na Mwandishi mkongwe Mussa Ally Bwakila na kuongezwa na Juma Mtanda ikijaribu kuangalia maisha ya Rais wa Uruguay na mustakabali wa Rais ajaye wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete.
José Alberto "Pepe" Mujica Cordano, aliyezaliwa Mei 20, 1935 ni Rais wa sasa wa Uruguay, ambaye hapo kabla alikuwa mpiganaji wa msituni wa kundi la Tupamaros na mfungwa wa kisiasa kwa zaidi ya miaka 13.
Kiongozi huyo anasifika kwa kutokuwa mpenda makuu na kuishi maisha yale yale wanayoishi Wananchi wake wa hali ya chini walio wengi.
Zaidi ya hayo hujitolea asilimia 90 ya msharara wake wa Dola 12,000 na marupurupu mengine kila mwezi kusaidia wahitaji, hasa wasiojiweza na wajasiriamali wadogo.
Mujica anaishi shambani kwake kwenye nyumba ya gharama nafuu ya mkewe Bibi Lucía Topolansky (ambaye ni mpiganaji mwenziwe wa zamani wa msituni na mmoja wa masenata wa chama tawala).
Akiwa na walinzi wasiozidi wawili, akitumia gari moja chakavu ya kizamani lenye thamani isiyofikia dola 2,000 Na kwa safari za hapa na pale mjini hutumia pikipiki ndogo.
Maisha yake ameamua kuyatoa kwa raia wake, hushirikiana nao kwenye safu za mstari wa mbele wa vita dhidi ya ujinga, umasikini na maradhi, hali inayolifanya taifa lake kuanza kuona mwangaza mpana wa maendeleo mwishoni mwa pango la ufukara, kupitia timu yake ya Ikulu na nje ya Ikulu iliyojipamba na sifa ya Uzalendo na Uwajibikaji, yenye sera na mipango inayotekelezeka inayolenga maendeleo endelevu kwa jamii husika.
“Watu huniita kuwa mimi ni Rais masikini kabisa Duniani, Bila shaka si kweli; Kiongozi masikini ni yule aliyejilimbikizia mali huku wananchi wake wakigubikwa na ufukara uliopea mipaka, naye akiendelea kuwanyonya na kutotosheka kabisa na alichonacho…” anaweka bayana Rais Mujica.
HAYO NI URUGUAY; Je hali ikoje kwa Tanzania tuitakayo ?.
Kwa ‘waliotangaza nia’ na ‘watakaotangaza nia’ ya Kushika mamlaka na madaraka kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais, wapo wenye sifa ya JOSÉ ALBERTO "PEPE" MUJICA CORDANO, RAIS MPANDA BAJAJI ?
TUNAHITAJI VIOPNGOZI AINA YA MUJIKA TUFIKE KULE TUNAKOTARAJIA KUFIKA.
JibuFuta