Vurugu kubwa zimetokea Zanzibar zikihusisha wafuasi wa kundi la Uamsho. Kituo cha Polisi kilivamiwa ili kumtoa kiongozi wa Uamsho aliyekamatwa kwa kuendesha mhadhara bila ya kuwa na kibali cha polisi.
Polisi walitumia mabomu kuwatawanya wananchi hao wenye hasira kali wakiwa na silaha za jadi km mapanga, marungu, mishale nk.
Kwa mujibu nwa taarifa za mitandaoni huko Zanzibar kumetokea kupiga mawe magari ya serikali huku wafanyakazi wa serikali wakijeruhiwa.
Picha hapo juu inaonesha gari la Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi mheshimiwa Khamis Musa aina ya Prado lenye namba SMZ 249A likiwa limepinduliwa, yeye mwenyewe hakuwemo katika gari.
Katibu huyo Mkuu bali alikuwemo dereva wake ambae mpaka sasa hali yake inaendelea vizuri, Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi. (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni