Serikali ya Nigeria imeteta vikali kuhusu tukio la polisi wa nchi hiyo kunaswa katika kanda video wakimtesa kinyama raia mmoja wa Nigeria mjini Cape Town.
Wizara ya mambo ya nje ya Nigeria imetoa kauli yake baada ya kanda hiyo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha polisi wakimpiga vibaya mwanaume huyo, kumvua nguo na kisha kumfunga kwa pingu.
Nigeria imetuma barua yenye ujumbe mkali kwa serikali ya Afrika Kusini ikitaka haki kutendeka kwa mwanamume huyo.Waliotekeleza unyama huo ni polisi na walinzi.
Polisi wawili wamekamatwa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanatuhumu polisi kwa ukatili, kukosa ujuzi wa kazi na ufisadi.
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Nigeria ilisema : "Ubalozi wa Nigeria utaendelea kutathmini kisa hicho hadi pale haki itakapotendeka,''
Tume ya polisi imesema kuwa polisi hao watafikishwa mahakamani kwa kosa hilo.
Takriban watu 17,000 raia wa Nigeria wanaishi nchini Afrika Kusini lakini waandishi wa habari wanasema kuwa kuna visa vingine vingi kama hivi dhidi ya wahamiaji haramu.
Mwaka jana raia wa Msumbiji Mido Macia alifariki baada ya kubururwa kwenye barabara na polisi akiwa amefungwa kwenye gari la polisi Mashariki mwa
Johannesburg.
Maafisa tisa wa polisi walifikishwa mahakamani na kesi yao ingali inaendelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni