ISIS INATESA WAKRISTO - OIC
Wapiganaji wa ISIS
Jumuiya ya kimataifa ya kiislamu amewalalamikia wapiganaji wa
kundi ISIS kile kinachodaiwa kuwanyima haki za kibinadamu wakristo waliopo
katika mji wa Masul nchini Iraq ambapo baadhi yao wamelazimika kuyakimbia makazi
yao.
Mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya kiislam OIC, Iyad Madani, kulazimika kukimbia
makazi yao kwa wakristo kwa sababu ya wapiganaji hao ni kinyume na misingi ya
dini ya kiislam inayosisitiza uvumilivu na ustahimilivu.
Maelfu ya Wakristo waliukimbia mji wa Mosul baada ya wapiganaji wa ISIS
kuwalazimisha kubadili dini na kuwa waislam, kulipa kodi ama kuuawa kama
wangekaidi.
Mwishoni mwa wiki ISIS walitangaza kuwa wanashikilia eneo jingine karibu na
Mosul (TK).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni