Baadhi ya wanawake na wasichana huko nchini Kenya wanatumia
sabuni inayodaiwa kurejesha usichana yaani 'ubikra'.
Sabuni hiyo inadaiwa kukaza misuli ya sehemu za uke na hivyo kuimarisha raha
wakati wa kushiriki tendo la ngono na mwanaume.
Baadhi ya wasichana waliohijiwa na BBC mjini Nairobi wamekiri kutumia sababu
hiyo na kusema kuwa imeweza kubana misuli ya uke na kurejesha hali ya
ubikira.
Hata hivyo mtaalam wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini Tanzania anasema
kutumia sabuni pamoja na kemikali nyingine kwenye uke ni hatari.
Mtaalam huyo amewashauri wanawake kuacha kutumia kemikali kwani pia inaweza
kuwaletea magonjwa mengine kama vile saratani (BBC)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni