Alhamisi, 25 Septemba 2014

SASA MBU KUANZA KUPAMBANA NA HOMA YA DENGUE

Watafiti wanaamini kuwa Mbu hao wenye viini watapambana na homa ya Dengue
Watafiti nchini Brazil, wameachilia maelfu ya Mbu wenye viini vya Bakteria ili kupambana na homa ya Dengue.
Wanatumai kuwa Mbu hao watazaana kwa haraka idadi yao ikiwa kubwa zaidi nchini Brazil na hivyo kuangamiza homa hiyo ya Dengue.
Mradi huu ni sehemu ya programu ambayo pia inafanyika nchini Australia, Vietnam na Indonesia.
Viini vya Bakteria vilivyotumika kuambukiza Mbu hao, hawana madhara kwa binadamu.
Programu hiyo iliyoanza mwaka 2012, kwa mujibu wa mmoja wa watafiti, Luciano Moreira, ambaye anaongoza utafiti huo.
Watafiti hao walitembelea mitaa minne mjini Rio, na kudadisi Mbu waliotolewa kutoka sehemu mbali mbali.
Mbu elfu kumi wataachiliwa kwenda katika maeneo ya watu kila mwezi kwa miezi minne.

'Viini vizuri vya Bakteria'
Viini hivyo vya Bakteria vinajulikana kama Wolbachiana na vinapatikana katika asilimia 60 ya wadudu.Vinafanya kazi kama chanjo kwa Mbu, ambao wana virusi vinavyosambaza homa ya Dengue, vinavyozaana mwilini.
Viini hivyo pia vinazuia kuzaana kwa Mbu wanaoeneza homa ya Dengue.
Utafiti huo, ulianza katika Chuo Kikuu cha Monash nchini Australia mwaka 2008.
Watafiti waliruhusu Mbu hao kunyonya damu kutoka kwenye mikono yao kuona ikiwa wanaweza kuambukiza homa ya Dengue.
Homa ya Dengue ilianza kuwa kero tena nchini Brazil mwaka 1981, baada ya kupotea kwa miaka 20.
Miaka 30 iliyofuata, matukio milioni saba vya maambukizi yaliripotiwa.
Brazil ndiyo nchi yenye matukio mengi vya maambukizi ya Dengue, huku watu milioni 3.2 wakiambukizwa na wengine 800 wakifariki kati ya mwaka 2009-2014

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni