Jumatano, 3 Septemba 2014

MZUNGU JELA MIAKA 17 KWA KUMUUA MSICHANA MWEUSI WA MIAKA 19






Theodore Wafer

Jaji mmoja nchini Marekani amemhukumu mwanamume mmoja kifungo cha miaka kumi na saba jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mwanamke mweusi ambaye hakuwa na silaha, na ambaye alikuwa akigonga mlango mkuu wa nyumba yake mapema asubuhi.

Theodore Wafer,a mbaye ni mzungu, alijitetea kua alikua akihofia uhai wake ndipo akajitetea kwa kumpiga risasi binti huyo mweusi aliyekuwa na miaka 19, Renisha McBride mjini Detroit.
Jaji huyo alimshutumu Theodore kwa maamuzi yake mabaya,l akini pia binti huyo hakustahili kufa. Binti Theodore alikuwa nagonga katika nyumba hiyo kuomba msaada baada ya kupata ajali ya gari.

Baada ya kufanyia uchunguzi mwili wa binti huyo walimkuta ana kiwango kikubwa cha pombe. Mauaji ya binti huyo yalizusha maandamano, na kifo chake kinafananishwa na kijana Andrew kutoka Florida Trayvon Martin aliyepigwa risasi mwaka 2012

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni