Washukiwa wanne wa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jengo la
Westgate wanaozuiliwa mjini Nairobi, wanadai kuwa wameteswa na walinzi wa
magereza kwa kukataa kuvaa sare zao za gerezani.
Washukiwa wengine 9 wanakabiliwa na tuhuma za ugaidi pia wansemekana kupata
majeraha mabaya.Tukio hilo, linasemekana kutokea wiki jana baada ya washukiwa hao kukataa kuva sare zao za gerezani kama wafungwa wengine.
Nchini Kenya, wafungwa wlaiopatikana na hati pekee yao ndio huvalia sare za gerezani. washukiwa hao ambao ni mchanganyiko wa wasomali wenye uraia wa Kenya na wasomali wahamiaji bado wako rumande.
Jamaa wa washukiwa wamekatazwa kuwaona lakini wakili wao sasa ana wasiwasi kuhusu afya ya washukiwa hao na tisho la wao kudhulumiwa na wafungwa wenzao.
Mahakama sasa inasema kuwa washukiwa hao watafikishwa mahakamani katika siku chache zijazo.
Kesi inayoendelea dhidi ya watuhumiwa hao wanne kuhusiana na madai ya kuhusika na shambulizi la Westgate bado haina ushahidi kuonyesha kuwa watu hao walihusika na kuwasaidia watu walioshambulia jengo la Westgate mjini Nairobi mwaka jana.
Hawajasemekana kufanya shamulizi hilo bali wanakabiliwa na tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la kigaidina kumiliki silaha zilizotumiwa kwa shambulizi la kigaidi.
Zaidi ya mashahidi 35 tayari wameshatoa ushahidi wao mahakamani huku wengine zaidi wakitarajiwa kufika mbele ya mahakama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni