Alhamisi, 26 Juni 2014

WAKIMBIA NYUMBA ZAO HUKO KENYA WAKIHOFIA MASHAMBULIZI

Mamia ya watu kutoka eneo la Wetu wamekimbia nyumba zao na kupiga kambi nje ya Kanisa la  African Inland Church (AIC) pamoja na maafisa wa wilaya kufuatia mauaji ya Jumatatu huko katika kijiji cha Kathaka Kairu village, Pandanguo sub-location.

Nusu ya watu wamepiga kambi nje ya kanisa hilo kwa mujibu wa taarifa za Mratibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wa eneo la Magarini na Kilifi Bwana Hassan Musa ambaye pia anasimamia eneo la wilaya ya Mpeketoni huko Lamu.

“Kuna kiasi cha familia 200 eneo la  AIC na katika ofisi ya DO WITU" alisema  Hassan Musa.

Aliongeza kuwa "Tunaandikisha watu katika kambi hizo mbili na tunasubiri serikali kuanzisha kambi hizo rasmi.”

 Mkuu wa Wilaya ya Mpeketoni Bwana Ben Maisori aliseam kuwa shule moja huko Pandanguo imefungwa baada ya walimu kuikimbia kufuatia mauaji hayo ya Jumatatu

 

Bwana Maisori alidai kuwa makabila hasimu mjini Lamu na maeneo ya jirani yanatumia mwanya huo kulipiza kisasi.

Wakimbizi hao wa ndani walisema wanaiomba serikali iwaongezee askari kwani  wana hofu kubwa.

Wakati huo huo Naibu Gavana ERic Mugo, pamoja na Mbunge Julius Ndegwa na mjumbe wa baraza la Mji Bwana James Njomo walisema kuwa Polisi ndio wanaosaidia eneo likitokea machafuko. Eneo la Mpeketoni limekuwa likikumbwa na visa vya mauaji na uharibifu wa mali siku za hivi karibuni. Watatu hao walisema hayo walipokuwa katika hospitali ya wilaya kupokea misaada kutoka kwa watu mbalimbali ili kusaidia wahanga wa tukio hilo.

Mwenyekiti wa Bandari nchini Kenya (KPA) bwana Danson Mungatana aliwaongoza mameneja wakuu wa KPA ambapo walichangi madawa na na fedha taslimu sh milioni moja ya Kenya. (Tukuo)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni