Nyani mmoja katika jimbo la Himachal Pradesh Kaskazini ya
India, amewagawia watu pesa taslimu kutoka mtini.
Taarifa zinasema kuwa watu waliokuwa wanajivinjari katika mji wa Shimla
jimboni humo, walianza kukimbia huku na kule wakiokota pesa zilizokuwa
zinarushwa na Nyani huyo kutoka juu ya mti kwa karibu saa moja.Nyani huyo aliingia katika nyumba hiyo kutafuta chakula lakini alipokosa chakula akaamua kutoweka na pesa.
Kuna karibu Nyani 300,000 katika eneo hilo. Jimbo la Shumla limekuwa makao kwa wanyama wengi.
Nyani aina ya Macaque, huonekana kama wanyama wa kuabudiwa na hivyo hulishwa na wakazi.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanyama hao, wamekuwa wakizozana na wakazi kwa sababu ya kuharibu mimema , kushambulia watu na hata kuwauma watoto.
Maafisa tayari wametangaza wanyama hao kuwa kero kubwa kwa wakazi.
Nyani huyo mwanzo alionekana akiwa ameketi juu ya paa la nyumba akiwa na bunda la noti kabla ya kuanza kuwagawia watu pesa hizo kwa kuwarushia.
watu walipoanza kukusanya pesa hizo, Nyani huyo alikimbilia kwenye mti mwingine.Lakini watu waliokuwa wanokota pesa hizo walimfuata kwani pesa haziachiki.
"Nyani alionekana kushtushwa na idadi ya watu waliokuwa wanamfuata lakini alipokimbilia kwenye mti mwingine, watu waliendelea kumfuata,'' alisema mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.
Pengine hili ni fundisho kwetu na kwa watu wengine kuwa nyani akija kwako ni vyema akakuta chakula (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni