kiongozi wa Sudan Kusini akibadilishan mkataba wa amani na kiongozi wa waasi
Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wamelaumiana kwa kuvunja
makubaliano ya kusitisha mapigano - masaa machache tu baada ya makubaliano kufikiwa.
Msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, alisema wapiganaji
wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu leo alfajiri.
Wapiganaji wamewashutumu wanajeshi wa serikali kuwa waliwashambulia katika
sehemu kadhaa katika majimbo ya Upper Nile na Unity.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa
kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha
zaidi ya watu milioni moja kuhama makwao (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni