Vidic akiifungia Manchester bao dhidi ya Bayern
Kulikuwa na mechi mbili za mkondo wa kwanza wa robo fainali ya
ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa Jumanne usiku, Manchester United
ya Uingereza ikikabana koo na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Bayern Munich ya
Ujerumani.
Nayo Barcelona ya Uhispania ikikabiliana na Athletico Madrid vilevile ya
Uhispania na kutoka sare ya 1-1..
Licha ya kuwa Bayern Munich ilikuwa imepigiwa upatu kutamba dhidi ya
Manchester United vijana wa pep Gardiola walikabiliwa na ukuta mrefu wa
Manchester uwanjani Old Traford.
Na walipopata fursa nahodha wa Manchester Nemanja Vidic alifunga bao maridadi
la kichwa baada ya kuunganisha vizuri kona kutoka kwa Wayne Rooney kunako dakika
ya 58 ya kipindi cha pili.
Gonga gonga ya Wajerumani ilizaa bao la Bastian
Schweinsteiger kunako dakika ya 66 iliwatunuku mabingwa hao watetezi bao
muhimu la ugenini kabla ya mkondo wa pili utakaochezwa huko Ujerumani .
Bila
shaka mashabiki na watani wa kocha David Moyes watakubaliana naye kuwa United
itajutia fursa aliopoteza Danny Welbeck alipokuwa ni yeye pekee dhidi ya kipa wa
Bayern Manuel Neuer .
United vilevile itamshukuru kipa David de Gea aliyefanya kazi ya ziada kuzuia
mashambulizi haswa kutoka kwa Arjen Robben.
Kutokana na sare hiyo sasa mkufunzi Pep Guardiola hana kibarua kigumu pale Man
United itakapozuru uwanja wa Allianz Arena wiki ijayo.
Mechi nyingine zitakazochezwa baadaye leo, Real Madrid ya Uhispania ikivaana na
Borussia Dortmund kutoka Ujerumani nayo Paris st Germain ikiikaribisha
wawakilishi wengine wa Uingereza Chelsea ya Uingereza katika uwanja wa Parc des
Princes(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni