Ajaribu kujizika kukwepa matatizo ya ndoa nchini Kenya
Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa kijiji cha
Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia kaburi na hata
kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha luninga cha KTN nchini Kenya, tukio hilo lililotokea
Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift
Valley
Mwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe
ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndio maana
akaamua kujitoa uhai.
Mwanamume huyo kwa jina Kipsang, alichimba kaburi hilo usiku na hata
kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na watoto wake walipokuwa wamelala. Matumaini aliyosalia nayo mwanamume huyo ni ya kwenda mbinguni
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na wasiwasi kuwa mwanamume huyo
alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri kwamba yeye na mkewe wamekuwa
wakikumbwa na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na
majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa matatu, hatimaye aliondoka
katika kaburi hilo baada ya wanakijiji kumsihi huku wazee wakiwataka watu
kupanda migomba ya Ndizi eneo alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi (TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni