Majeshi ya Sudan Kusini yanajiandaa kupambana na waasi katika
mji wa Bor, Rais Salva Kiir amesema
Rais Kiir ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba majeshi yapo tayari na
kuongeza kuwa mashambulizi yalichaleweshwa ili kuruhusu raia wa Marekani
kuondolewa katika eneo hilo.
Bor, ni eneo lililokuwa mgogoro ambalo lipo ndani ya jimbo la Jonglei ambalo
lilimeangukia mikononi mwa waasi siku ya jumatano.
Takribani wiki imepita tangu mapigano ya kikabila yaanze na kusababisha hofu
kwa raia. Maafisa ya shirika la misaada wanaelezea eneo hilo limekuwa na matukio
ya umwakigaji damu pamoja na mauaji.
Mapema Majeshi ya Sudan Kusini yamethibitisha kuwa Bentiu, mji wenye utajiri
wa mafuta katika jimbo la limeangukia mikononi mwa wapiganaji wanaoungwa mkono
na Makamu wa Rais aliyestaafu Riek Machar
Rais Kiir , kutoka kabila la kubwa nchini humo la Dinka, mwezi Julai alimfuta
kazi Bwana Machar anatokea jamii ya Nuer.
Rais Kiir anamtuhumu Bwana Machar kwa kufanya jaribio la kumpindua, jambo
linalopigwa vikali na Machar.(Chanzo BBC)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni