Jumatatu, 23 Desemba 2013

UNYAMA ZAIDI WAJITOKEZA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe James Lembeli

Unyama zaidi umebainika katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili baada ya kudaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Francis Miti, alijihifadhi kwenye hoteli moja nje ya wilaya yake.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, James Lembeli akisoma ripoti hiyo bungeni juzi alisema Operesheni Tokomeza Ujangili, ulisababisha hofu miongoni mwa wananchi na viongozi na baadhi yao kuyakimbia makazi. Lembeli alisema watuhumiwa, walikamatwa, walipekuliwa na kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo.
"Baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi, madiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji na watumishi wa Serikali, walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza," alisema Lembeli(P.T)



Aliongeza; "Watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za siri bila ridhaa yao."
Lembeli alitoa mfano kuwa Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanawe wa kiume (11) akishuhudia huku akilazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake.
Alisema mwanamke mmoja wa Babati (jina tunalo) alidai kuvuliwa nguo na kulazimishwa kufanya mapenzi na wakwe zake, pia kuingizwa chupa sehemu zake za siri.
Aidha, baadhi ya wanawake walidai kubakwa na kulawitiwa huku wilayani Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na Askari wawili wa Operesheni Tokomeza Ujangili mida ya usiku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni