Jumatatu, 23 Desemba 2013

NDEGE YAPATA AJALI AFRIKA YA KUSINI

Sehemu ya Jengo iliyoharibiwa na Ndege jijini Johannesburg
Ndege iliyokuwa imebeba zaidi ya abiria 200 imeharibu sehemu ya jengo katika uwanja wa ndege wakati ilipokuwa ikijiandaa kuruka katika uwanja wa ndege wa mjini Johannesburg, Afrika kusini.
Ndege inayomilikiwa na shirika la ndege British Airways iliyokuwa ikielekea London ilikuwa ikiambaa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa OR Tambo wakati ubawa wake wa kulia ulipogonga sehemu ya jengo na kusababisha Watu wanne waliokuwa ndani ya jengo hilo kujeruhiwa.
Picha zimeonesha ubawa wa ndege aina ya Boeing 747 ikiwa imejikunja.Mamlaka ya usafiri wa anga ya nchini Afrika kusini imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikiambaa kwenye njia nyembamba.
Ajali hiyo ilitokea jumapili mwishoni mwa juma lililopita.Msemaji wa mamlaka ya anga, Phindiwe Gwebu amesema kuwa marubani walipewa maelekezo lakini walikosea na kupita njia ambayo ndege hiyo haikupaswa kupita.
Hakuna yeyote aliyejeruhiwa miongoni mwa waliokuwa ndani ya ndege hiyo, isipokuwa wafanyakazi wanne waliokuwa katika jengo lililoharibiwa ambao wanaelezwa kupata majeraha lakini wanaendelea vizuri hivi sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni