Jumatatu, 23 Desemba 2013

TRENI YAJERUHI WATU KADHAA KIBERA, NAIROBI

Watu zaidi ya kumi walijeruhiwa wakati mabehewa manne ya mizigo yalipopinduka  na kuangukia juu ya vibanda kando ya njia ya relieneo la Kibera jijini Nairobi  ambapo wanaishi watu wengi .

Waokoajii wanajaribu kutafuta nafasi katika mtaa wenye nyumba zilizosongamana sana, ili kuleta mashine ya kunyanyua mabehewa ili kuwafikia wale walionasa.

Mabehewa yalianguka juu ya vibanda vilivyo karibu na njia ya reli.

Magazeti yanaarifu kuwa kazi za uokoaji zimekuwa ngumu kwa sababu watu wengi wamezonga eneo hilo.
 Waokoaji wana wasiwasi kuwa pengine watu kadhaa wamenasa chini ya treni iliyopinduka katika mitaa ya Kibera, Nairobi - eneo la watu maskini.
Vibanda vya Kibera vimejengwa karibu sana na njia ya reli
Sehemu ya njia ya treni inayopita Kibera

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni